Polisi nchini Uganda wanakabiliwa na shutuma za kuwatesa washukiwa wa mauaji, ya aliyekuwa naibu mkuu wa polisi Andrew Kawessi pamoja na kuwakamata watoto.Hata hivyo Rais Yoweri Museveni amewatetea polisi hao akisema kuwa,washukiwa hao wanahitaji kipigo zaidi ya walichopata.
Shutuma dhidi ya polisi zinafuatia malalamiko ya washukiwa walipofikishwa mbele ya hakimu, wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya aliyekuwa naibu wa mkuu wa polisi Felix Kawesi.
Washukiwa wameieleza mahakama kuwa polisi wanawapiga, pamoja na mateso mengine wakiwalazimisha kutoa taarifa.
