Polisi Dar es Salaam wasitisha wito wa kumuita Tundu Lissu

In Kitaifa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM leo October 2, 2020, limesitisha wito wa kumtaka mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania CHADEMA Tundu Lissu kufika kituo cha polisi na badala yake kuendelea na ratiba za kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Jana Alhamisi tarehe 1 Oktoba 2020, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lilimuandikia barua ya wito Lissu likimtaka afike katika ofisi zake leo Ijumaa saa 3:00 asubuhi kujibu tuhuma zake.  Leo tarehe 2 Oktoba 2020, SACP Lazaro Mambosasa,  Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, amesema jeshi hilo limesitisha wito wake kwa Lissu likidai, limeona busara Lissu aendelee na ratiba yake.

“Jeshi la Polisi limesitisha wito huo na kumtaka Tundu Lissu kuendelea na kampeni zake za Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.”

“Jeshi la polisi limeona ni vema kutumia busara kumuacha Lissu kuendelea na ratiba zake kipindi hiki cha kampeni na kwa kuwa tayari IGP Sirro alishatoa maelekezi kwa Lissu kuripoti Kituo cha Polisi Moshi Mkoa wa Kilimanjaro. Hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalum limesitisha wito huo,” amesema Kamanda Mambosasa. 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu