Polisi Rwanda wakanusha kumzuia mwanamke aliyetaka kuwania Urais.

In Kimataifa, Siasa

Polisi nchini Rwanda wamekanusha kwamba wanamzuilia mwanamke aliyetaka kuwania urais katika uchaguzi uliofanyika mapema mwaka huu.

Taarifa zilikuwa zimeenea mitandao ya kijamii nchini humo kwamba polisi wamemkamata Diane Shima Rwigara na mamake.

Msemaji wa Polisi ya Rwanda Theos Badege amewaambia waandishi wa habari  kuwa polisi walifanya upekuzi nyumbani kwake kama sehemu ya upelelezi wa mwanzo kuhusu makosa anayotuhumiwa yeye na familia yake ambayo ni pamoja na kosa la kughushi nyaraka na kukwepa kulipa kodi.

 

Taarifa zilikuwa zimesema kuwa watu wasiojulikana ambao walikuwa na silaha lakini walivalia mavazi ya kiraia walivamia nyumbani kwa mwanasiasa huyo mapema leo Jumatano.

 

Familia yake inasema kufikia sasa bado mwanamke huyo na mamake hawajulikani waliko.

Diane Rwigara alikataliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu ambapo Rais Paul Kagame alishinda kwa kura nyingi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu