Polisi wa Ufaransa wamemfyatulia risasi na kumjeruhi mtu mmoja mjini Paris, ambaye alimshambulia afisa wa polisi kwa kutumia nyundo.
Tukio hilo limeripotiwa kufanyika nje kidogo ya kanisa kuu la Notre Dame nchini humo.
Kufuatia tukio hilo kanisa hilo lilidhibitiwa kwa muda, na hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia ndani au kutoka nje kwa kipindi cha saa moja.
Ufaransa ipo katika hali ya hatari, kufuatia msururu wa mashambulizi ya kigaidi katika miaka ya hivi karibuni
