Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

In Kimataifa

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuu
Jackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wa
washirika wawili ambao bado hawajakamatwa.


Uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanaharakati na mwanamitindo wa
LGBTQ umechukua sura mpya huku polisi wakiwakamata washukiwa
wengine watatu huku mshukiwa mkuu Jackton Odhiambo akikiri
kumuua mwanamitindo huyo.

Watatu hao walikamatwa Jumamosi kwa kubeba sanduku la chuma
ambalo mwili wa Chiloba ulipatikana.
watu watatu waliokamatwa ni watoto wawili na mwanamume mmoja
ambaye polisi wanaamini kuwa anaweza kutoa taarifa muhimu kuhusu
mauaji hayo yaliyotikisa taifa.


Msemaji wa polisi Resla Onyango alithibitisha kuwa maafisa wa
upelelezi pia wamekamata gari linaloaminika kubeba maiti ya
mwanaharakati huyo hadi ilipotupwa.


Katika ungamo la kutisha, mshukiwa alifichua kwamba alimuua
mwanaharakati na mwanamitindo wa LGBTQ kwa usaidizi wa marafiki
wawili ambao bado hawajafahamika.

Jackton pia alifichua kuwa walikuwa kwenye uhusiano na waliishi
pamoja na marehemu kama mume na mke.
Mshukiwa huyo aliyejikiri aliongezea kuwa alimuua Chiloba kama
kulipiza kisasi kwa kumsaliti katika uhusiano wao.

OCPD wa Langas John Odhiambo alibainisha kuwa msako umeanzishwa
ili kuwapata washirika wawili wa Jackton ambao bado hawajapatikana.
Majirani walivutiwa na harufu mbaya iliyokuwa ikitoka katika nyumba
hiyo ambayo mshukiwa mkuu alishirikiana na marehemu.

“Aliwaambia majirani ni panya aliyekufa ambaye alikuwa ananuka
walipotafuta kujua nini kilikuwa kinanukia kutoka kwa nyumba

waliyokuwa wakiishi,” mkuu wa DCI kaunti ya Uasin Gishu Peter
Kimulwo alisema.

Majirani waliambia polisi kwamba walimwona Jackton akiwa na
sanduku la chuma siku moja kabla ya mwili wa Chiloba kupatikana
kwenye sanduku la chuma ambalo lilitupwa Halingham karibu na
Kipkaren.

Msimamizi wa nyumba aliyokuwa akiishi chiloba amby anafahamika
kwa jina la alex nyamwea amefichua kuwa rafiki yake ambaye ni
mshukiwa mkuu katika mauaji ya chiloba alihama kutoka nyumba hiyo
tarehe 4 mwezi huu na alimpgia simu kupitia simu ya marehemu
kumfahamisha kuwa ana hama.


Na baada ya mwili wa marehemu kukutwa umetupwa tarehe 3 mwezi
huu mshukiwa alionekana akibeba vyombo vya nyumba na kuhama
hapo walipokuwa wakiishi pamoja na kwa mujibu wa msimamizi wa
nyumba hizo mshukiwa huyo alionekana akiisafisha nyumba hyo

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Somaliland yagundua Mafuta

Jamhuri iliyojitangaza ya Somaliland imetangaza kugunduliwa kwa kisima cha mafuta katika eneo la Salhayey eneo la Marodi-Jeh, wizara yake

Read More...

WAKAZI WA ARUSHA WAHIZWA KUTUNZA AMANI YA JIJI LA ARUSHA AMBALO NI KITOVU CHA UTALII NCHI

Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi Wananchi wa jiji la Arusha wamehimizwa kutunza amani na utilivu wa jiji hilo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu