Polisi wanaochuguza shambulio la bomu katika ukumbi wa burudani wa Manchester Arena wameacha kutoa taarifa kwa Marekani baada ya taarifa kuvuja katika vyombo vya habari , BBC imefahamu.
Maafisa Uingereza walighadhabishwa wakati picha zinazo onekana kuonyesha masalio kutoka shambulio hilo zilipochapishwa katika gazeti la New York Times.
Hili linajiri baada ya jina la mlipuaji Salman Abedi lilipofichuliwa kwa vyombo vya habari vya Marekani saa chache baada ya shambulio hilo lililosababisha vifo vya watu 22 wakiwemo watoto, na kuwajeruhi wengine 64.
Theresa May anatarajiwa kumuelezeaDonald Trump wasiwasi wake katika kikao ha jumuiya ya kujihami Nato baadaye.
Polisi Manchester inatarajia kurudi katika uhusiano wa kawaida wa kubadilishana intelijensia hivi karibuni, lakini kwa sasa kuna “hasira kubwa” BBC inafahamu.
Kikosi hicho kinachoongoza uchunguzi kinawasilisha taarifa kwa taasisi ya kitaifa ya kupambana na ugaidi, ambacho nacho kinasambaza taarifa serikalini na kwasababu ya makubaliano ya kubadilishaa intelijensia inasambaza pia kwa Marekani, Australia, Canada na New Zealand.
Kwa jumla watu 8 wanauziwa kufuatia shambulio hilo lililotekelezwa na raia mzaliwa Manchester Abedi, mwenye umri wa miaka 22 kutoka familia walio na asili kutoka Libya.
Imeibuka pia watu wawili waliomtambua Abedi akiwa katika chuo kikuu walipiga simu tofuati kuonya polisi kuhusu misimamo yake ya itikadi kali
