Polisi yatoa kauli kwa dada aliyeibiwa Mil 20.

Mfanyabiashara ambaye ni Wakala wa miamala ya simu na
kibenki Mkoani Manyara Tatu Athuman,amejitokeza na
kuthibitika kuwa ndiye aliibiwa Milioni 20 baada ya Wahalifu
kuvunja nyumbani kwake na baadaye kukamatwa na Polisi
wakiwa nyumba ya kulala Wageni.


Kamanda wa Polisi ktk mkoa wa Manyara George Katabazi
amesema wamejiridhisha kuwa,Mfanyabiashara huyo ndiye
aliyeibiwa fedha hizo,huku wakiendelea na kubaini mtandao huo
wa uhalifu na kuwataka Wafanyabihashara kuweka Walinzi
katika maeneo yao ya biashara.

Exit mobile version