Rafa Benitez amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Everton, ambayo inatajwa kuwa mbioni kumtimua kazi meneja wao wa sasa Ronald Koeman, kufuatia matokeo mabaya yanayoendelea kuwaandama.
Benitez alikua wa kwanza kwenye orodha ya mameneja wanaopigiwa chepuo kuchukua nafasi ya ukuu wa benchi la ufundi huko Goodison Park, kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha katika ligi ya England.
Benitez mwenye umri wa miaka 57 ametangaza msimamo huo, kwa kuamini bado ana nafasi ya kuendelea kudhihirisha ubora wake akiwa na kikosi cha Newcastle Utd, ambacho alikirejesha ligi kuu msimu uliopita kikitokea ligi daraja la kwanza.
Benitez anaendelea kukumbuka ka kazi nzuri aliyoifanya akiwa na liverpool mwaka 2005, na kufikia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa barani Ulaya kwa kuifunga AC Milan.
