Rafael Nadal ang’ara katika michuano ya Us Open.

In Kimataifa, Michezo

 

Mcheza tenesi namba moja kwa ubora duniani Rafael Nadal ameshinda taji la 16 la Grand Slam na taji la tatu katika michuano ya US  Open baada ya kumshinda Kelvin Anderson kwa seti 6-3,6-3 na 6-4.

Imekuwa rahisi kwa Nadal kushinda Grand Slam bila kuwa na upinzani mkubwa kutokana na kutokuwepo kwa wakali kama Novack Djokovick, Andy Murray na Rodger Federer.

 

Rafael Nadal ilikuwa wazi asingepata upinzani mkubwa kwani wachezaji wote walioko katika 20 bora ya viwango vya tenesi walikuwa tayari wametupwa nje ya michuano hiyo na Nadal alichuana na mchezaji anayeshika nafasi ya 28 katika viwango vya tenesi duniani.

 

Hii ni Grand Slam nyingine kwa Nadal baada ya kushinda Grand Slam mwaka 2013 na inatimiza idadi ya Grand Slam 16 kwa Nadal huku akishinda mbele ya mashabiki wanaompenda kama mwenyeji wa hapo mjini NewYork.

 

Nadal sasa anakuwa na US Open 3 na kuwa na Grand Slam 16 akimkaribia kinara wa Grand Slam Rodger Federer ambaye hadi sasa ameweka kabatini jumla ya Grand Slam 19.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu