Raia wa Uganda wenye matumaini ya kusafiri nje ya taifa hilo wamekwama baada ya taifa hilo kuishiwa pasi za kusafiria.
Afisa mmoja wa wizara ya Wizara ya mambo ya Ndani aliiambia DW kwamba wana deni wanalopaswa kulipa kwa wachapishaji nchini Uingereza.
Tatizo hilo linatarajiwa kudumu kwa takribani mwezi mmoja. Na katika kipindi hiki wizara inatoa pasipoti kwa dharura za matibabu tu.
Kamishna wa Udhibiti wa Pasipoti amesema ongezeko la maombi limesababishwa na idadi kubwa yawatu wanaokwenda kufanya kazi Mashariki ya Kati, ambapo kwa siku kitengo hicho kimekua kikitoa pasipoti 700.
Mwaka jana wizara ililazimima kusimamisha utoaji wa pasipoti na kurefusha pasipoti baada kwisha kabisa.
