Raia wa Venezuela wamepiga kura yenye utata ya kulichagua bunge maalum.

Raia wa Venezuela wamepiga kura yenye utata ya kulichagua bunge maalum litakalo ibadilisha katiba ya nchi hiyo. Hata hivyo uchaguzi huo kwa kiwango kikubwa ulisusiwa na wananchi na uligubikwa na ghasia zilizosababisha mauaji.

Kwa mujibu wa habari watu wasiopungua tisa waliuwawa katika mji mkuu wa Caracas na sehemu nyingine za nchi hiyo. Rais Nicolas Maduro amesema uchaguzi huo una lengo la kuutatua mgogoro wa kiuchumi na kisiasa nchini Venezuela lakini wapinzani wa serikali wanasema kura hiyo itaua demokrasia katika taifa hilo la Kusini mwa Amerika.

Marekani, Colombia, Panama,Peru na mashirika kadhaa ya kimataifa yamesema hayatotambua matokeo ya kura hiyo.

 

Exit mobile version