Raila Odinga aituhumu Tume ya Uchaguzi kwa kuandaa mbinu chafu.

In Kimataifa

Mgombea urais wa Kenya anayeungwa mkono na umoja wa vyama vya upinzani wa NASA, Raila Odinga ameituhumu Tume ya Uchaguzi nchini humo kwa kuandaa mbinu chafu dhidi yake ya kuchapisha karatasi za ziada za kupigia kura.

Mwanasiasa huyo mkongwe amedai kuwa mbinu hiyo pia ilitumika wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013, na kwamba ndio sababu kuu ya Tume hiyo kusisitiza Kampuni ya Al Ghurair kuchapisha karatasi, kitendo ambacho kambi hiyo ya upinzani imekipinga mahakamani.

Akizungumza  wakati akiupokea ugeni wa viongozi kutoka Kiambu jijini Nairobi kwa lengo la kuanza ziara ya kuwatembelea wapiga kura leo, Odinga alikejeli wito uliotolewa na Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wake, William Ruto kumtaka mgombea wake mwenza Kalonzo Musyoka kumtelekeza na kujiunga na kambi la Jubilee.

Odinga alisisitiza kuwa NASA imepanga kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii nchini Kenya na kwamba Jubilee hawatashinda uchaguzi wa Agosti 8.

Odinga amesema NASA ni sura ya Kenya na  Nchi inakwenda kushuhudia mapinduzi ya kijamii na kiuchumi,na kuwa wapo kwenye hatua za kufanya mageuzi ya nchi huku akiwaeleza wapinzani kuwa kwa sasa  mabadiliko yanakuja na Jubilee hawawezi kushinda akisisitiza kuwa wanakwenda  kuzungumzia mambo yanayowaletea madhara Wakenya kwani wana suluhisho.

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Kenya alieleza kuwa NASA wataanzisha safari Julai 7 mwaka huu, Uhuru Park itakayoongozwa na maombi na kisha kuelekea kwenye uwanja wa Kamukunji kwa ajili ya sikukuu ya Sabasaba.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

NACTIVET YASIMAMISHA MAFUNZO CHUO CHA MBEYA TRAINING..DC MALISA AAGIZA KUFANYIWA UHAKIKI VYUO VYOTE WILAYA YA MBEYA

Wazazi Wanafunzi na wahitimu wa chuo cha Mbeya training wameiomba serikali iwasaidie kurudishiwa stahiki zao mara baada ya kubainika

Read More...

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE NOVEMBA 7, 2023

Manchester United na Newcastle United zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki, 20, ambaye mkataba wake unamalizika Juni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu