Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli, leo ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ Lugalo Jijini Dar es Salaam, na kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo.
Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata alishambuliwa na watu wenye silaha, wakati akiingia nyumbani kwake eneo la Ununio, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, imeeleza kuwa Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana mchana na kisha kupelekwa katika hospitali ya jeshi Lugalo kwa matibabu.
Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe, amemueleza Rais Magufuli kuwa Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.
