Wengi mtakuwa mnakumbuka tamko la mheshimiwa Rais wa Jamuhuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, alilolitoa akiwa ziarani mkoani Pwani.
Rais alisema katika Serikali ya Awamu ya Tano hakutakuwa na mwanafunzi atayepata ujauzito akiwa shuleni, atakaeruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Tamko hilo liliibua hisa tofauti kwa wadau mbalimbali hasa watetezi wa haki za wanawake na watoto wa kike, wakisema inawanyima watoto wa kike haki ya kupata elimu, kwa sababu wengi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni hawakusudii bali wengine hubakwa.
Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko ambaye ni mmoja wa wadau wanaofanya jitihada kumlinda mtoto wa kike, ambaye amekuwa na hisia tofauti na tamko la Rais Magufuli na kumtaka kulikiria kwa mara nyingine.
