Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku 2.
Leo Rais Magufuli ameianza ziara hiyo kwa kuongoza sherehe za ufunguzi wa daraja la waenda kwa miguu la Furahisha,lilipo katia wilayani ya Ilemela mkoani humo.
Katika hotuba yake rais Magufuli amezunmgumzia miradi mingine mikubwa inayofanyika mkoani humo, na kuwataka wakazi wa Mwanza kuhakikisha wanalitunza daraja hilo.
Pia Rais magufuli amewathibitishia wakazi wa mwanza kuwa, chini ya uongozi wake yaliyoshindikana lazima yawezekane, likiwepo la kuupanua uwanja wa ndege wa Mwanza.
