Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzuru nchini leo, katika ziara ya rasmi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa rais John Pombe Magufuli.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Tanzania Augustine Mahiga, amesema ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara,na kuangazia maswala mbali mbali ya maendeleo.
Rais Zuma ataandamana na mawaziri sita, pamoja na wafanyibiashara kadhaa kutoka Afrika Kusini.
Atakuwa nchini kuanzia leo tarehe 10 hadi 13, akitarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake rais Magufuli ikulu ya rais jijini Dar es salaam.
