RAIS John Magufuli amekutana na timu ya wataalamu wa masuala ya umeme na ujenzi, wa miundombinu ya mabwawa ya maji kujadili mradi mkubwa wa kuzalisha umeme mwingi hapa nchini.
Rais amekutana na wataalamu hao na kujadiliana kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme, katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 za umeme.
Rais amekutana na wataalamu hao ikiwa ni utekelezaji wa nia yake ya kuhakikisha mradi huo unaanza kujengwa haraka iwezekanavyo, na kuzalisha umeme mwingi utakaosaidia kuharakisha maendeleo hapa nchini, hususani ujenzi wa viwanda.
Leo Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn anawatuma wataalamu wake waliojenga mradi mkubwa wa bwawa la maji la kuzalisha umeme nchini Ethiopia.
