Rais John Magufuli amesema kitendo cha kampuni kadhaa za uchimbaji madini kushirikiana na baadhi ya watumishi wa umma nchini, kufanikisha utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi na kuwaacha Watanzania wakifa na kuteseka kwa umaskini, ni unyama usiovumilika na umefika mwisho.

In Kitaifa

Rais John Magufuli amesema kitendo cha kampuni kadhaa za uchimbaji madini kushirikiana na baadhi ya watumishi wa umma nchini, kufanikisha utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi na kuwaacha Watanzania wakifa na kuteseka kwa umaskini, ni unyama usiovumilika na umefika mwisho.

Aidha amesema hata kitendo cha taasisi za umma kuwabana wafanyabishara wadogo, kwa kushindwa kujisajili na kulipa kodi huku taasisi hizo zikishindwa kuyabana makampuni yanayoingiza faida za mabilioni, huku yakiwa hayajasajiliwa, ni unyama uliokithiri.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana baada ya kupokea ripoti ya Kamati maalumu ya kuchunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusiana na mchanga wa madini unaosafirishwa nje ya nchi.

Aidha ripoti hiyo  iliyobainisha kuwa, kupitia mikataba michafu, Tanzania imepoteza takriban shilingi trilioni 108, katika kipindi cha miaka 19 toka mwaka 1998 hadi 2017, kupitia usafirishaji wa makinikia maarufu mchanga wa dhahabu.

Kutokana na hali hiyo, Rais ametoa maagizo mazito likiwamo la kutaka mawaziri wote wa nishati na madini waliohusika kuliingiza taifa katika mikataba iliyolingamiza taifa kiuchumi, wahojiwe popote walipo.

Moja ya mapendekezo ya Kamati hiyo iliyoongozwa na Profesa Nehemiah Osoro (Mwenyekiti) ilishauri Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waliokuwa mawaziri, wanasheria wakuu wa serikali na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za mikataba, na makamishina wa madini.”

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

RC MBEYA AFANYA UZINDUZI ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA (NIDA)

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho

Read More...

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu