Rais John Magufuli amesema kwa sasa hakuna mchanga wa madini utakaotoka kwenda nje ya nchi, huku akiitaka kampuni ya uchimbaji madini nchini Acacia kutubu na kukubali makosa yake, kama inataka kuendelea kufanya biashara nchini.

Rais John Magufuli amesema kwa sasa hakuna mchanga wa madini utakaotoka kwenda nje ya nchi, huku akiitaka kampuni ya uchimbaji madini nchini Acacia kutubu na kukubali makosa yake, kama inataka kuendelea kufanya biashara nchini.

Ameagiza mamlaka zinazohusika kuiita kampuni hiyo na kabla ya jambo lolote, inapaswa kuilipa serikali fedha kwa kuwa imefanya udanganyifu kwa muda mrefu, wakishakubali hayo tunaweza kukaa kwa makubaliano.

Ametoa kauli hiyo baada ya kupokea ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa kuchunguza mchanga wa madini uliokuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi, huku akiwataka wanasheria kuungana pamoja kwaajili ya maslahi mapana ya Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kuunda timu ya wanasheria waaminifu ambao watapitia na kuzifanyia marekebisho sheria zote zinazohusu mikataba ya madini ili zipelekwe bungeni kwaajili ya kujadiliwa na kufanyiwa marekebisho.

Amesema kuwa sheria hizo zinapaswa zipelekwe bungeni hata kama ni kwa bunge kuongezewa muda ili ziweze kujadili nakufanyiwa marekebisho kwa maslahi mapana ya Taifa.

Aidha ameelezwa kushangazwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kushindwa kuwa na rekodi ya usafirishwaji wa dhahabu pamoja na Wizara ya Nishati na Madini kufanya kazi na kampuni ya Acacia bila kujua kama haijasajiliwa.

 

 

Exit mobile version