Rais John Magufuli amewataka wananchi wenye asili ya burundi waliopo nchini Tanzania ,warudi makwao kwa kuwa Rais wao Pierre Nkurunziza, ameshawahakikishia kuwa kuna amani ya kutosha.
Ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera ,katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika viwanja vya Posta, baada ya kupokea ugeni kutoka nchini Burundi wa rais huyo pamoja na baraza lake la mawaziri mchana wa leo ,uliyokuja kwa mazungumzo ya kiuchumi.
Aidha, Rais Magufuli ameunga mkono ombi la Rais wa Burundi aliyowataka wananchi wake warundi kwao wakaijege kwa pamoja nchi hiyo kwa kuwa hakuna shida ya aina yoyote katika kipindi hiki.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amemthibitishia Rais Nkurunziza kuwa Tanzania, itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa majirani zake wote waliopo ndani ya Afrika Mashariki ndani ya SADC pamoja na nchi ya Burundi.
