Rais John Magufuli leo anatarajiwa kupokea ripoti ya Kamati ya Pili ya wachumi na wanasheria, iliyochunguza madini yaliyopo kwenye makontena yenye mchanga wa madini.

Rais John Magufuli leo anatarajiwa kupokea ripoti ya Kamati ya Pili ya wachumi na wanasheria, iliyochunguza madini yaliyopo kwenye makontena yenye mchanga wa madini.

Anapokea ripoti hiyo ikiwa ni takribani siku 19 tangu alipokabidhiwa ripoti ya mchanga wa madini, iliyoibua madudu na hata kumlazimu kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa kwa vyombo vya habari, Rais Magufuli atakabidhiwa ripoti hiyo leo asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.

Kamati hiyo ilichunguza aina na viwango vya madini, yaliyomo kwenye mchanga wa madini uliomo ndani ya makontena, yaliyokuwa yamezuiliwa bandarini na Serikali yasisafirishwe kwenda nje ya nchi.

Baada ya kupokea, ripoti hiyo ilionesha mchanga uliokuwa unachunguzwa, ulikuwa na wastani wa kiasi cha thamani kati ya Sh bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani wa chini na Sh trilioni 1.439 kwa kutumia viwango vya juu.

Kutokana na taarifa hiyo, Rais Magufuli aliivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), na kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo kutokana na kutosimamia ipasavyo, mchakato mzima wa usafirishaji mchanga wenye madini nje ya nchi na hivyo kuisababishia nchi hasara kubwa.

Aidha, mbali na kutengua uteuzi wa Waziri Muhongo, alivunja Bodi ya TMAA na kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wake. Rais Magufuli pia aliviagiza vyombo vya dola, kuwachunguza na kuwachukulia hatua watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na wengine waliohusika na kushindwa kusimamia vema mchakato mzima wa usafirishaji wa mchanga wenye madini nje ya nchi.

Exit mobile version