RAIS John Magufuli mgeni rasmi Julai Mosi katika ufunguzi wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara

In Kitaifa

RAIS John Magufuli atakuwa mgeni rasmi Julai Mosi katika ufunguzi wa Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ,maarufu Sabasaba yanayosimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yanayoanza rasmi Juni 28 hadi Julai 8, 2017 yakishirikisha makampuni toka nchi zipatazo 30.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho hayo vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam jana, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema maonesho ya mwaka huu yamelenga zaidi kusaidia wajasiriamali wadogo ili kuifikisha Tanzania katika uchumi wa viwanda.

Amesema Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Ukuzaji wa biashara kwa maendeleo ya viwanda,’ kwa sababu wanaamini biashara ndiyo inayokuza viwanda na bila kuuza hakuna ukuaji wa viwanda.

Mwijage amesema kila siku ya maonesho imetengwa kwa shughuli maalumu ya kumsaidia mshiriki kujiimarisha kibiashara, zipo siku za mazungumzo baina ya wafanyabiashara, siku za kukutana wafanyabiashara wa ukanda huu wa Afrika Mashariki na siku ya kujadili bidhaa.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo ameeleza  banda la bidhaa za ngozi litakuwa na shughuli maalumu,u ya kueleza faida ya bidhaa zitokanazo na ngozi pamoja na Gereza la Karanga kueleza azma ya kutengeneza soli za viatu na kuzisambaza nchini.

Awali akimkaribisha Waziri Mwijage, Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Edwin Rutageruka amesema washiriki watumie maonyesho hayo kutangaza bidhaa zao badala ya kufikiria kuuza lakini pia wabadilishane ujuzi na wafanyabiashara wa kimataifa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu