Rais Magufuli aagiza kufungiwa kwa benki na kampuni za simu.

In Kitaifa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ameagiza mamlaka husika kuzichukulia hatua ikiwamo kuzifungia kampuni za simu na benki ambazo zitashindwa kuanza kutumia mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki ifikapo mwisho wa mwaka huu 2017.
“Kwa kampuni za simu au benki zitakazoshindwa kutekeleza agizo hili, taratibu husika zifanyike. Ikiwezekana makampuni hayo au benki hizo zifungiwe kufanya kazi nchini” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo mjini Dodoma katika hafla ya ufunguzi wa tawi la benki ya CRDB lililopo katika jengo la LAPF-Dodoma.
Rais amezitaka benki zote pamoja na makampuni ya simu ambayo yanataka kuendelea kufanya biashara hapa nchini kuhakikisha kuwa wanajiunga na mfumo huu wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki kabla ya kufika mwisho wa mwaka huu wa 2017.
“Kwa taarifa nilizo nazo ni benki chache tu ambazo tayari zimejiunga na mfumo huu wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki. Benki na kampuni nyingi za simu bado hazijajiunga na mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki.  Benki na Kampuni zote za simu zinazotaka kufanya biashara Tanzania zihakikihshe zinajiunga na mfumo huu kabla ya mwaka huu (2017) kuisha,” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameagiza fedha kiasi cha shilingi 100 milioni alichopewa kama zawadi na Benki ya CRDB zitumike kujenga wodi ya wagonjwa katika hospitali ya Dodoma na kutaka wodi hiyo iitwe ‘wodi ya CRDB’ kama ishara ya heshima kwa benki hiyo.
Akiikabidhi hundi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rais Magufuli ameonya wahusika wote kutumia vizuri fedha hizo ili kuhakikisha ujenzi wa wodi hiyo unakamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachofaa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu