Rais Magufuli aanza ziara ya siku tatu Mkoa wa Pwani.

In Kitaifa

RAIS John Magufuli leo anaanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Pwani na anatarajia kuzindua viwanda vitano.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam jana, katika ziara hiyo Rais Magufuli atazindua viwanda vikubwa vitano ambavyo ni kiwanda cha vifungashio (Global Packaging Co. Ltd) na kiwanda cha matrekta (Ursus-TAMCO Co. Ltd).

Pia atazindua kiwanda cha chuma (Kiluwa Steel Group), kiwanda cha kukausha matunda (Elven Agric Company) na atafungua kiwanda cha vinywaji baridi (Sayona Fruits).

Pamoja na hayo, pia atazindua mradi wa maji wa Ruvu pamoja na barabara ya Bagamoyo – Msata ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara iliyoandaliwa.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu