Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine TAWIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Eblate Ernest Mjingo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI).

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Mjingo alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Tiba ya Wanyamapori na Huduma za Maabara wa TAWIRI, na anachukua nafasi iliyoachwa na Dkt. Simon Mduma ambaye amestaafu.

Uteuzi wa Dkt. Mjingo unaanza leo tarehe 29 Septemba, 2020.

Exit mobile version