Rais Magufuli amuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kutoa kibali cha ujenzi wa kituo cha Uchunguzi wa Maradhi.

Rais John Magufuli amemuagiza Mkurugenzi wa Manisapaa ya Moshi kutoa kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Uchunguzi wa maradhi , kilichoombwa na mwananchi mmoja mkoani humo  ili aweze kuendelea na ujenzi huo, kutokana na kutopewa kibali hicho kwa muda mrefu.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amesema kutokana na Serikali kuzuia unywaji wa pombe aina ya viroba ,idadi ya vifo katika mkoa wa Pwani imepungua kutoka 80 hadi 20, na hata ajali za pikipiki maarufu Bodaboda nazo zimepungua nchini.

Aidha, Rais Magufuli ametaka uongozi wa Wilaya ya Hai kufanya kazi bila kutishwa na madiwani, ikiwa ni pamoja na kubadili sheria ndogondogo wilayani humo ili kupunguza kero za utitiri wa ushuru, kwa wananchi.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo wakati alipokutana na viongozi wa dini wa mkoa wa Kilimanjaro, Vyama vya Siasa na watendaji wa Serikali mkoani humo, na kula nao chakula cha mchana kilichoandaliwa na mkoa wa Kilimanjaro

Raisi  Magufuli yupo Mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya kikazi na natarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maaadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo kitaifa yanaadhimishwa Mkoani Kilimanjaro.

Exit mobile version