Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemfuta kazi aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO), Balozi Hassan O Gumbo Kibelloh.
Kufuatia utenguzi huo, Rais Magufuli amemteua Gregory George Teu kuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo ya (KADCO),Na uteuzi huu unaanza leo October 16 2017.
Nyumba za ibada zakumbwa na bomoabomoa …
Mhandisi wa Tanroads ambaye anasimamia zoezi la ubomoaji wa nyumba, Jonson Rutechula ametangaza idadi ya nyumba za ibada 24 zinatarajiwa kubomolewa leo ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayoanzia Kimara hadi Kiluvya.
Ubomoaji wa nyumba hizo za ibada ni mwendelezo wa uboamoaji wa nyumba takribani 1300 za wakazi wa maeneo hayo zinazodaiwa kujengwa ndani ya mita 121.5 ya barabara hiyo.
Ambapo nyumba zaidi ya 1000 zimebolewa mpaka sasa, amesema kwa siku ya leo kazi maalumu itakuwa ni kubomoa nyumba za ibada.
Aidha shughuli za ubomoaji wa nyumba zimekamilika kwa asilimia kubwa ,zimesalia nyumba za ibada tu.
Kazi ya ubomoaji itaanza mapema asubuhi ya leo kuanzia eneo la Kimara hadi Kiluvya.
