Rais Mgufuli aagiza Watumishi 9,932 waliogushi vyeti waondolewe mara moja sambamba na kukatwa mishahara yao.

In Kitaifa

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.JOHN MAGUFULI, amepokea taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma  inayoonyesha uwepo wa watumishi waliogushi vyeti 9,932 na hivyo kuagiza kuondolewa kwenye ajira zao Mara moja.

RAIS MAGUFULI amefikia maamuzi hayo mara baada ya kupokea taarifa hiyo katika ukumbi wa chimwaga uliopo ndani ya chuo kikuu cha DODOMA {udom}, ambapo pia ameagiza kusitishwa kwa mishahara yao ya mwezi huu, pamoja na kuondolewa kwenye orodha ya majina iliyopo hazina na kusisitiza kuwa atakaye kaidi kuondoka hadi tarehe 15 mwezi may mwaka huu, afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Awali  akiwasilisha taarifa hiyo waziri wa nchi ofisi ya rais,utumishi na utawala bora ANGELAH KAIRUKI, amesema kuwa zoezi hilo liliwahusisha watumishi wa umma pekee wakiwemo makatibu wakuu,watendaji na maofisa wa ngazi mbalimbali za serikali, na kuwa zoezi hilo halikuwahusisha viongozi wa kisiasa katika utumishi wa umma wakiwemo wabunge,mawaziri,wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na madiwani kwani uteuzi wa nafasi zao ,hufanyika kwa kuwa na sifa ya kujua kusoma na kuandika pekee.

Kwa upande wake waziri wa elimu,sayansi na teknolojia na ufundi JOYCE NDALICHAKO, amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuachana na njia za mkato kwani tayari serikali imeziba njia hizo ,hivyo kuwasihi  wanafunzi wote katika taasisi za  elimu ya juu waliojiunga kwa kugushi vyeti kujisalimisha mapema.

Mbali na zoezi la mh.rais kupokea taarifa hiyo ya uhakiki wa vyeti kwa wa watumishi wa umma , pia amezindua maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa CHUO KIKUU CHA DODOMA {UDOM}

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mkuu mpya wa chuo cha Arusha asimikwa.

Chuo kikuu cha Arusha kimemsimika mkuu mpya wa chuohicho wakati wa mahafali ya 16 ambayo yamefanyika chuonihapo.  Mkuu aliyeachia nafasi

Read More...

Naibu Waziri Silinde atoa maagizo mazito Musoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe David Silindeamemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma VijijiniMkoa wa Mara, Msongela Palela

Read More...

Waziri mkuu abaini madudu ya ajabu mkuranga.

Waziri mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa,janaalifanya mkutano maalaum katika Wilya ya Mkuranga ambapoamebaini mambo kadhaa,likiwemo la watumishi wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu