Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anawasili Mkoani Tanga leo Agosti 3, 2017 kwa ajili ya uzinduzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Mara baada ya kuwasili Mheshimiwa Raisi alimpa fursa Diwani wa Kata ya Msata kueleza changamoto ikiwamo kero ya Maji ambayo ni kero kubwa kwa Wananchi hao.
Kata hivyo diwani huyo amemweleza Mheshimiwa Raisi Magufuli kuwa hospitali ya Wilaya ambayo imetengewa kiasi cha shilingi Milioni 500,bado haijaendelea mpaka sasa hali ambayo inawapelekea wananchi kutafuta huduma za afya maeneo mengine kutokana na Uhaba wa Fedha kutoka Serikali.
Aidha raisi Magufuli amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi na kusema kuwa Wameanza kufanyia Ahadi alizoahidi ikiwa ni Pamoja na Maji,Umeme Vijijini ambao umekwishafanikiwa na kuahidi suala la maji litakuwa historia katika eneo hilo.
Uzinduzi huo unatarajiwa kutafanyika Agosti 5, 2017.
