Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron leo anatarajiwa kutangaza jina la waziri mkuu wa taifa hilo.
Lakini litaidhinishwa na bunge la Ufaransa baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa bunge mwezi ujao.
Na kama chama kingine kitajinyiakulia wingi wa viti, atapaswa kutaja waziri mkuu miongoni mwa wabunge wa chama hicho na kutakuwa na hatari ya kupoteza udhibiti katika ajenda za siasa za ndani.
Mpaka wakati huu Macron hajaonesha ishara yoyote ni nani ambae atamchagua.
Vyombo vya habari vya ufaransa vimetaja wagombea kadhaa, miongoni mwa hao yupo Edouardo Philippe, meya muhafidhina wa eneo la pwani la Le Havre nchini Ufaransa.
