Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli anaongoza mamia ya watu katika hafla ya kitaifa ya kumuaga rais mstaafu wa taifa hilo Benjamin Mkapa ambaye aliaga dunia usiku wa kuamkia Ijumaa.
Toka Jumapili mwili wa Marehemu Mkapa umekuwa ukiagwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Hii leo ilikuwa ni zamu ya viongozi wakuu wa taifa pamoja na wageni kutoka nje ya Tanzania kuaga.
Kabla ya viongozi hao kupewa nafasi ya kutoa salamu za rambi rambi waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Prof Palamagamba Kabudi, alisoma wasifu wa hayati rais mstaafu awamu ya tatu, Benjamin Mkapa,na kusema enzi za uhai wake, Mkapa alimuoa Anna na kubahatika kupata watoto wawili wa kiume, Stephano na Nicholas.
Bada ya wasifu huo viongozi wa nje waliopata nafasi ya kutoa salamu za rambi rambi akiwemo waziri mkuu wa Burundi General Bunyoni Gwame.
Pia walikuwepo mabalozi 41 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, lakini kwa niaba yao balozi wa Comoro Aphmada Elbadui Phaki, alipewa nafasi ya kutoa salamu za rambi rambi kwa niaba yao.
Kwa upande wake Rais Magufuli katika hotuba yake akayaeleza baadhi ya mambo yaliyofanya na rais Benjamini Mkapa enzi ya uhai wake hata baada ya kustaafu.
Licha ya kuyazumgumza mambo mengi yaliyofanywa na Rais Mkapa, Rais Magufuli amesema kuwa Mzee Mkapa ni shujaawake kwani hata alipopatwa na shida ama kupambana na changamoto mbalimbali hakumwacha.
Msikie hapa rais John Pombe Magufuli akizungumza hayo,haliiliyopelekea kushindwa kujizuia hadi kutoa machozi.
Mzee Benjamini Mkapa anatarajiwa kuzikwa kesho Kijijini kwake Lupaso,mkoni Mtwara kusini mwa Tanzania.
