Rais Museven wa Uganda atetea uongozi wake na kuwashutumu wanaomuita Dikteta.

 Raia nchini Uganda wamekuwa wakisambaza mahojiano ya hivi karibuni ya rais Museveni na shirika la habari la Aljazeera ambapo alizungumzia maswala kadhaa.

Katika mahojiano hayo, alitetea kipindi chake cha miongo mitatau kama rais wa Uganda na kuwashutumu wale wanaomuita dikteta, akisema kuwa huenda amekuwa dikteta mzuri kwa sababu amekuwa akichaguliwa na wananchi mara tano.

Alizungumzia kufungwa kwa mwanaharakati Stella Nyanzi ambaye anazuiliwa kifungoni amesema kuwa  hana haki ya kuwatusi wengine.

Haki zinaenda sambamba na majukumu, iwapo unajua chochte kuhusu demokrasi. Alikataa kuingizwa katika mazungumzo ya vita vilivyokuwa katika jimbo la magharibi la Kasese,ambapo vikosi vya usalama vilikabiuliana na walinzi wa mfalme wa eneo hilo, mzozo uliowacha makumi kufariki na wengine wengi kuuawa akisema kuwa ni swala ambalo linaangaziwa mahakamani”.

Exit mobile version