Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amezindua maadhimisho ya miaka 10 tangu Burundi ijiunge na Umoja wa Afrika Mashariki EAC, na kuahidi kuihimiza nchi yake ifungamane zaidi na umoja huo.
Jumuiya hiyo inayoundwa na nchi 6 yaani Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Sudan Kusini na Uganda, bado haijatimiza muungano wa kifedha na shirikisho la kisiasa ambayo ni hatua ya mwisho ya mafungamano ya umoja huo.
Rais Nkurunziza amesema Burundi inatakiwa kusawazisha sheria zake hasa zile za usimamizi wa kodi na kanda hiyo ili isiwe vizuizi kwenye mchakato wa kutimiza mafungamano kamili ya umoja huo.
