Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan, leo Aprili 05 amefungua mkutano wa kitaifa wa haki,
amani na maridhiano Tanzania.
Mkutano huo utakaofanyika kwa siku 2 utahusisha kumkabidhi
uenyekiti wa TCD Abdulrhaman Kinana, baada ya Zitto Kabwe
kumaliza muda wake.
Rais Samia Suluhu Hassan
amewataka wajumbe wa mkutano
huo,kuweka mbele utaifa na wazingatie mazingira yaliyopo hapa
nchini katika yale watakayoenda kuyajadili.
Katika hatua nyingine Rais Samia amesema kuwa,Tanzania
haitajengwa na mtu mmoja au chama kimoja bali itajengwa na
Watanzania wote.
Hivyo kwa pamoja nia lazima wajadili mambo yote iwe sera,
sheria na dira ni lazima vijadiliwe na wote kama Watanzania.