Rais Samia awaapisha viongozi alioteuliwa.

In Kitaifa

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan,leo amewaapisha mawaziri watatu huku akitoa angalizo
kwa mambo matatu yanayoweza kumkwaza katika utekelezaji
wa majukumu yao,utii katika maelekezo wanayopewa na
Serikali, utunzaji wa siri za Serikali na utetezi wa katiba ya nchi
bila kubagua upande.


Rais Samia anatoa maelekezo hayo leo Oktoba 3 2022 Ikulu
jijini Dar es Salaam wakati wa viapo vya wateule hao baada ya
mabadiliko madogo ya baraza lake la mawaziri kwa
kuwahamisha wawili, kumuondoa mmoja na kumrejesha
Angella Kairuki bungeni kisha kumteua kuwa waziri.


Rais Samia amemuapisha Kairuki ambaye alimteua kuwa
mbunge wa Bunge la Tanzania kisha kumteua kuwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

(Tamisemi) huku akimweka kando Balozi Liberata Mulamula
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.


Pia amemuapisha Dk Stergomena Tax aliyechukua nafasi ya
Balozi Mulamula pamoja na Innocent Bashungwa aliyekuwa
Waziri wa Tamisemi aliyemuhamishia Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa JKT kuchukua nafasi ya Dk Tax.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu