Rais Samia awahapisha viongozi aliowateuwa.

In Kitaifa

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan leo amewaapisha viongozi aliowateuwa katka ukumbi
wa Ikulu Chamwino jijini Dodoma.


Taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatano Julai 20,
2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu Bi Zuhura
Yunus,imesema kuwa uteuzi huo umeanza jana.


Viongozi walioapishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi
la Polisi Simon Sirro,aliyeteiliwa kuwa Balozi wa Tanzania
nchini Zimbabwe.


Nafasi ya Sirro imechukuliwa na Camillus Wambura ambaye
amepandishwa cheo na kumteuliwaa kuwa Inspekta Jenerali na
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP.

Pia Rais Samia amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa
Polisi ACP Ramadhan Kingai,kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai DCI.


Baada ya zoezi la kiapo kukamilika,Waziri wa mambo ya ndani
ya nchi Eng Hamad Masauni alipata wasaa wa kuzungmza
machache na kutoa neno la shukrani kwa Rais Samia.

Kwa upande wake Rais Samia akizungumza baada ya vingozi
hao kula kiapo amewataka kwenda kufanya kazi na kuzingatia
kwa mujibu wa kiapo walichokula,lakini pia akaeleza sababu ya
kufanya mabadiliko.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu