Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia
Suluhu Hassan,leo amehitimisha ziara yake katika mkoa wa
Singida,ambapo amezindua Mradi wa Maji Tinde kutoka Ziwa
Victoria na amepokea taarifa ya Mradi wa Umeme Vijijini REA
awamu ya tatu mzunguko wa pili, na kuzungumza na wananchi
wa Wilaya ya Iramba Eneo la Shule ya Msingi Shelui.
Kabla ya kwenda kumsikia Mhe Rais Kile alichokizungumza,
namsogeza kwako mbunge wa jimbo la Iramba ambaye ni pia ni
waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba,ambaye alipata wasaa
wa kutoa neno kwa Rais samia kwa niaba ya wananchi wa jimbo
lake.
Kwa upande wake Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akizungumza
na wananchi,ameelezea ziara yake mkoani humo ya siku tatu
nay ale yaliyofanyika katika mkoa wa Singida.
Jambo lingine ambalo Rais Dkt Samia alilolizungumza ni kuwa
serikali inaendelea na mchakato wa kuchukua hatua za haraka ili
kukabiliana na changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara,
pia akasema serikali itaendelea kuzitatua changamoto mbali
mbali nchini baadhi akizitaja kutoka katika jimbo la Iramba.
