Rais (TLS) awahimiza wafanyakazi kuhakikisha wanashikamana na kudai haki zao za msingi.

In Kitaifa
raisi wa chama cha wanasheria tanganyika (TLS) Tundu Lissu amewahimiza wafanyakazi nchini kupitia vyama vyao ,vya wafanyakazi kuhakikisha wanashikamana kudai haki zao za msingi, ili tija wanayotoa iendane na mapato.
Bw. Lissu ameitoa rai hiyo mjini Dodoma, wakati alipokutana na wanachama wa shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi (TAFETU), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.
Lissu ambaye pia ni rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki, amesema umefika wakati sasa kwa shirikisho hilo la (TAFETU) kudai haki za wanachama wao, badala ya kuziomba, kwa sababu ni haki yao.
Mwenyekiti wa taifa wa (TAFETU) Bw. Albert Machumu, amesema hakuna haja waajiri kuvichukia vyama vya wafanyakazi nchini, kwa kuwa vyama hivyo vinatekeleza majukumu yake, kwa mujibu wa sheria za nchi.
Shirikisho hilo la (TAFETU) linaundwa na vyama sita, huku kukiwa na vyama vingine 22 visivyo chini ya shirikisho hilo wala lile la (TUCTA).

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu