Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aagiza madaktari mia258 kuajiriwa.

In Afya, Kitaifa

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JOHN MAGUFULI ameagiza kuwaajiri madaktari mia 258, pamoja na wataalam wengine kumi na moja11, waliojitokeza kuomba ajira nchini Kenya na kukidhi vigezo vilivyohitajika

Hatua hiyo ya kuwaajiri madaktari hao imefikiwa na Serikali baada  ya baadhi ya madaktari nchini Kenya ,kuwasilisha pingamizi mahakamani kuitaka Serikali ya nchi  yao kusitisha kuajiri   madaktari mia tano 500 kutoka Tanzania ,ambao waliombwa na nchi ya Kenya.

Akizungumza na waandishi wa Habari Bungeni mjini Dodoma,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema,kufuatia uamuzi huo,majina ya madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti  ya Wizara hiyo.

Amesema kuwa rais amefikia uamuzi huo baada ya mahakama nchini kenya kuweka pingamizi hilo serikali ya Tanzania,imeamua madaktari hao ambao walionyesha utayari wa kufanya kazi katika mazingira yoyote waatiwe ajira hapa nchini badala ya Nchini Kenye kama ilivyokuwa hapo awali.

Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya afya dk ULISUBISYE MPOKI amewatoa hofu watanzania juu ya ugonjwa wa amofilia kwa kusema kuwa ugonjwa huo si wa  ajabu na mpya kama wengi wanavyodhani bali ni ugonjwa wa hatari kwani ni wa kurithi ambao husababisha shida katika damu kuganda na kuwa  wapo wataalumu  wengi amabao wanaweza kushughulikia tatizo hilo
Waziri Ummy walimu ameongeza kuwa wizara ilipokea maombi 496 na baada ya kuyachambua madaktari 258 ,ndiyo waliokidhi vigezo vilivyokuwa vimewekwa,pamoja na hayo amesema kuwa bado tanzania ipo tayari kuipatia nchi ya kenya madaktari wengine pindi wakiwahitaji.

Mwezi machi mwaka huu Serikali ya Tanzania ilikubali ombi la Kenya la kuisaidia nchi hiyo  madaktari mia tano 500, watakaosaidia kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari katika vituo vyake vya tiba kufuatia kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu