Rais wa Madagascar: Dawa ya Mitishamba ya kutibu Corona Inakataliwa Kwakua inatoka Afrika.

In Kimataifa

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amesema kwamba wakosoaji wa dawa ya mitishamba ambayo haijajaribiwa ambayo anaipigia debe kuwa tiba ya Covid-19 inaonyesha tabia ya ubwenyenye ya mataifa ya magharbi dhidi ya Afrika.

Shirika la Afya duniani limeonya dhidi ya kutumia dawa ambazo hazijafanyiwa majaribio. Dawa hiyo ya rais Rajoelina haijapitia majaribio ya wanadamu.

Muungano wa Afrika pia umesema kwamba inataka kuona data ya kisayansi kuhusu uwezo na usalama wa dawa hiyo kwa jina Covid-Organics.

”Iwapo ingekuwa ni taifa la Ulaya ambalo liligundua dawa hiyo , je kungekuwa na wasiwasi? sidhani”, bwana Rajoelina alisema katika mahojiano na shirika la habari la ufaransa 24.

‘Dawa’ ya Madagascar yahamasisha tiba za jadi za KiafrikaMadagascar imeripoti wagonjwa 193 wa Covid-19 na hakuna kifo hata kimoja. Dawa hiyo ilifanyiwa majaribio watu 20 katika kipindi cha wiki tatu, mshauri wa rais huyo aliambia BBC wakati bidhaa hiyo ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita – hatua ambayo haiendani na muongozo wa WHO kuhusu majaribio.

WHO inasema kwamba vipimo na utafutaji wa watu waliokaribiana na wagonjwa ndio njia bora ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
Licha ya madai hayo , mataifa kadhaa ya bara Afrika ikiwemo Nigeria, Guinea-Bissau , Equitorial Guinea na Liberia , tayari yameagiza dawa hiyo inayozalishwa kutoka kwa mmea wa pakanga – mti unaotumiwa kutengeneza dawa ya malaria pamoja na miti mingine ya Malagasy.

WHO imesema kwamba Waafrika wanahitaji kupata dawa ambayo imepitia majaribio ya kuridhisha hata iwapo inatoka katika tiba za kitamaduni.

Katika mahojiano hayo ya runinga, bwana Rajoelina alisema wanasayansi wa Afrika hawafai kudharauliwa.

Lakini kuna ushahidi kuonyesha kwamba dawa ya Covid-Organic ina uwezo.

Mkutano wa wataalam 70 wa dawa za kitamaduni Afrika umeafikiana na kwamba dawa zote zinapaswa kufanyiwa majaribio miongoni mwa binadamu , kulingana na shirika la Afya duniani tawi la Afrika ambalo lilichapisha katika twitter.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza,

Read More...

Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuuJackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wawashirika wawili ambao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu