Bwana Trump aliambia chombo cha habari cha NBC kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.
Bwana Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya, maafisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.
Bwana Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliopingwa na Mrithi wa Comey.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo , Bwana Trump aliambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza bwana Comey iwapo alikuwa akimchunguza.
Rais huyo pia alipinga maelelezo ya ikuu ya Whitehouse kwamba alimfuta bwana Comey baada mapendekezo kutoka maafisa wakuu wa wizara ya haki.
