Rais wa Marekani Donald Trump amewaambia washirika wa Marekani katika shirika la kujihami la mataifa ya Magharibi, Nato, mjini Brussels kwamba washirika wote ni lazima wagharimie sehemu yao ya gharama ya matumizi ya kijeshi.

Ni “kiasi kikubwa sana cha pesa” ambacho hakijalipwa, alisema, na kukariri wasiwasi ambao umekuwepo kwamba Marekani imekuwa ikilipa fedha zaidi kuliko washirika wake.

Bw Trump pia amelaani shambulio la bomu la Manchester lililotekelezwa Jumatatu na kusema kwamba ugaidi shari ukomeshwe.

Alitoa wito wa kuwepo kwa kipindi cha kimya kwa heshima ya watu 22, watu wazima na watoto, waliouawa katika “shambulio hilo la kikatili”.

Bw Trump pia ameonya kuhusu hatari ambayo inaletwa na kuruhusiwa kwa watu kuhama bila kudhibitiwa na pia hatari inayotokana na urusi.

Kabla ya kuzuru makao makuu ya Nato, Bw Trump alikutana na viongozi kadha wa EU kwa mara ya kwanza, wakiwemo rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Exit mobile version