Rais wa Somalia ameyataka mataifa makubwa duniani kumsaidia kupambana na magaidi.

Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed ameyataka mataifa makubwa duniani kumsaidia kupambana na magaidi , rushwa na umasikini, katika mkutano wa kimataifa wenye lengo la kuimarisha taifa hilo lililoharibiwa kwa mizozo chini ya uongozi mpya.

Mohamed Abdullahi ameuambia mkutano huo mjini Landon kwamba taifa hilo lililoharibiwa kwa mizozo linaweza kuneemeka kutokana na uwezo wa jadi wa Wasomali wa kufanya biashara iwapo linaweza kuzuwia kitisho cha njaa , uharamia na itikadi kali ya kiislamu.

Mkutano huo wa siku moja , uliohudhuriwa na viongozi mbali mbali duniani, unataka kufikiwa makubaliano mapya kati ya Somalia na mtandao wa waungaji wake mkono wa kimataifa kuharakisha maendeleo katika masuala ya usalama, maendeleo na uchumi ifikapo mwaka 2020.

Taifa hilo la Afrika mashariki lenye matatizo , ambalo mara kwa mara limekuwa juu katika faharasa ya mataifa dhaifu , limepata rais , waziri na bunge jipya mwaka huu na mkutano huo unalenga kuweka uthabiti katika kundi hilo la viongozi

Exit mobile version