Rais wa Somalia atangaza vita dhidi ya Al Shabab, awataka kujisalimisha.

In Kimataifa

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi “Farmajo” ametangaza vita dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab.

Farmajo ambaye amekuwa rais kwa miezi minne, ameongeza kuwa anatoa siku 60 kwa wanamgambo hao kujisalimisha.

Amefafanua kuwa ikiwa watajisalimisha, watapewa mafunzo ya kijeshi, watapewa elimu na kuajiriwa na serikai ya Mogadishu.

Kauli hii ya kiongozi huyu wa Somalia inakuja siku moja baada ya shambulizi la bomu mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine.

Amesisitiza kuwa maafisa wa usalama wamejipanga ipasavyo kuhakikisha kuwa mashambulizi ya Al Shabab hayatokei tena na wanakabiliwa ipasavyo.

Hivi karibuni, rais Farmajo aliwabadilisha maafisa wa usalama katika idara ya ujasusi katika juhudi za kukabiliana na Al Shabab.

Rais huyo ameyasema haya mjini Mogadishu ikiwa amevalia sare za kijeshi pamoja na Waziri wake Mkuu Hassan Ali Khayre, na kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuunga mkono juhudi za wanajeshi.

Kundi la Al Shabab ambalo lilianza mashambulizi yake nchini Somalia mwaka 2006, limesababisha mamia ya watu kupoteza maisha nchini Somalia na katika nchi jirani kama Kenya na Uganda.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu