Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi “Farmajo” ametangaza vita dhidi Al-Shabab

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi “Farmajo” ametangaza vita dhidi ya kundi la wanamgambo la al-Shabab.

Image result for Mohamed Abdullahi "Farmajo"
Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi “Farmajo”

Ametoa pia msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo hao, akiwataka kujisalimisha, ili wapate mafunzo, ajira na elimu.

Hi ni baada ya shambulizi la kujitoa mhanga kutokea karibu na jengo moja la serikali mjini Mogadishu ambapo watu 7 waliuawa pamoja na misururu ya kutekwa nyara kwa wafanyakazi wa kutoa misaada katika taifa hilo linalokumbwa na ukame.

Mashambulizi yamekuwa ya mara kwa mara na vikosi vyote nchini Somalia vimekuwa katika hali ya tahadhari ili kukabiliana na tisho lolote kwa usalama.

Pia amesema kuwa amewafanyia mabadiliko maafisa wa vyeo vya juu kwenye idara ya ujasusi na polisi ili kujiandaa katika vita dhidi ya al-Shabab.

Exit mobile version