Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ametangaza hali ya hatari kwa muda wa miezi mitatu katika jimbo la Gogrial, ambako mapigano yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa, kati ya wanamgambo kutoka koo za Apuk na Aguok za kabila la Dinka, analotokea Kiir.
Msemaji wa serikali amesema hapo jana.
Michael Makuei, ambaye pia ni waziri wa habari, amesema jeshi litapewa mamlaka maalum kuzuia mapigano katika jimbo hilo la Gogrial, na kwamba haki za raia zitasitishwa, licha ya kwamba rais hajatangaza ni haki gani zitaathirika.
Makuei alisema watu wapatao 70 waliuawa katika mapigano ya mwezi Mei.
Makuei amesema hali ya hatari pia inahusu katika maeneo jirani ya Tonj, Wau na Aweil mashariki.
