Rais wa Sudan kusini asitisha mpango wa kutembelea Makao Makuu ya jeshi jijini Juba.

In Kimataifa

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amesitisha mpango wa kutembelea Makao Makuu ya jeshi jijini Juba.
Mapigano yanaendelea kushuhudiwa nchini Sudan Kusini kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Riek Machar.
Ripoti zinasema kuwa, rais Kiir alikuwa ameanza safari ya kwenda katika makao hayo makuu Kaskazini mwa jiji kuu la Juba lakini alipofika katikati ya safari yake, aliamua kusitisha ziara yake.
Jeshi la Sudan Kusini limeendelea kushutumiwa na waangalizi wa Umoja wa Mataifa kwa kuendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya waasi na kusababisha maelfu ya raia w anchi hiyo kuyakimbia makwao.
Umoja wa Mataifa unasema mwaka huu pekee, watu elfu 95 wamekimbia makwao kwa sababu ya mapigano yanayoendelea.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu