Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema raia wake hawajutii uamuzi wao wa kupiga kura ya kutaka uhuru wao, licha ya kuwepo mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo changa.
Bwana Kiir alikuwa akizungumza hayo katika maadhimisho ya miaka sita ya Uhuru kutoka Sudan.
Sherehe rasmi ziliahirishwa kutokana na vita na hali mbaya ya uchumi.
Bwana Kiir amesema imefika wakati wa kujifunza kutokana na makosa ya zamani na kuungana kuijenga Sudan Kusini.
Maelfu ya watu wamekufa, na mamilioni wamehama makazi yao, tangu mgogoro huo ulipoanza mwezi Desemba mwaka 2013.
