Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema nchi yake haitarudi nyuma katika vita dhidi ya magaidi na wapiganaji wengine wa kijihadi nchini Mali na katika eneo la Sahel.
Macron ametoa kauli hii nchini Mali baada ya kuwatembelea wanajeshi wa Ufaransa katika kambi yao ya Gao Kaskazini mwa nchi hiyo.
Akiwa na rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita, Macron ameongeza kuwa Ujerumani pia itaendelea na nchi yake kuhakikisha kuwa magaidi hao wanashindwa.
Aidha, amesema kuwa ushirikiano wa Ufaransa na Ujerumani ni muhimu sana barani Ulaya katika maswala ya usalama lakini pia kulisaidia bara la Afrika.
Ufaransa imewatuma wanajeshi wake 1,600 Kaskazini mwa Mali kupambana na magaidi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Hii imekuwa ni ziara ya kwanza ya rais huyu mpya barani Afrika.
