Rais wa Uganda Yoweri Mueveni amevitaka vikosi vya usalama kuwacha kuwatesa wahalifu ikiwa wamekuwa wakifanya hivyo.
Kwa njia ya barua kwa maafisa wa ngazi za juu serikalini akiwemo waziri wa masuala ya ndani, amesema kutumia mateso kunaweza kusababisha mtu asiye na makosa kukiri na hivyo sio njia bora, ya kupata ushahidi ambao unaweza kutumika mahakamani.
Amesema kuwa Uganda imekabiliana na changamoto mbaya za kiusalama ,kuliko tishio kutoka kwa wahalifu wanaotumia pikipiki maarufu kama boda boda.
